matukio burudani injili uimbaji maisha sanaa muziki maigizo habari maajabu vichekesho maendeleo mafanikio uchumi lugha maono mahubiri nyimbo biblia siasa

Apr 30, 2012

BABA SOLLY MAHLANGU NDANI YA SAMA MUSIC AWARDS TAREHE 30/04/2012 AMENYAKUA TUZO

BABA SOLLY MAHLANGU TENA KWENYE SAMA YAANI SOUTH AFRICA MUSIC AWARD AKIIBUKA MSHINDI KATIKA KIPENGELE CHA BEST TRADITIONAL FAITH MUSIC ALBUM

CHINI: BABA SOLLY MAHLANGU AKIWA KATIKA MOJA YA PICHA HUKU AKIIMBA NA WATAZAMAJI

MAHOJIANO YA MWANZONI KABLA YA EVENT HII YALIKUWA HIVI:
 

MTN HOSTING SHUGHULI NZIMA YA SAMA (SOUTH AFRICA MUSIC AWARD) LOGO

KIZURI SIKU ZOTE CHAHITAJI MAANDALIZI. HAPA NI VIJANA WAKIFANYA MAANDALIZI YA TUKIO LENYEWE

 
Pamoja na vipengele vingi sana kwenye hizi tuzo zinazotolewa na MTN hizi ni baadhi ya gospel Music categories ambazo zilishindaniwa na walioshindanishwa ni kama ifuatavyo:
 
BEST CONTEMPORARY FAITH MUSIC ALBUM
walioshindani ni:
Joe Niemand-Ek Sal Nie Bang Wees Nie
Martin PK-Man On A Mission
Swazi Dlamini-Gospel Meets Jazz – Live In Durban
The Plain Truth-We Are The Shining Ones
We Will Worship-The Movemeant Begins

BEST TRADITIONAL FAITH MUSIC ALBUM

walioshindanishwa ni:
Kgotso-New Dawn
Nqubeko Mbatha-Forever I'll Worship
Sfiso Ncwane-Kulungile Baba
Solly Mahlangu-Mwamba Mwamba
Soweto Spiritual Singers


Best Traditional Faith Music Album

Solly Mahlangu for Mwamba Mwamba

IYELELE TEAM INAMPONGEZA SANA BABA SOLLY MAHLANGU KWA SABABU KUU MBILI:
-KWA KUKUBALI KUFANYA NYIMBO ZA INJILI KWA KUTUMIA UTAMADUNI WA NYIMBO ZA KIAFRICA
-KWA KUTUMIA LUGHA ZOTE ZA AFRICA BILA KUBAGUA ( KUMBUKA MWAMBAMWAMBA NI NYIMBO YA KISWAHILI) AMBAYO NDIYO IMEMPA USHINDI.

Kifupi ni kuwa watu wengi ambao ni waafrica hawajajua uthamani wa lugha zao na tamaduni zao ambazo zikitumiwa vyema zinamtukuza Mungu vile zilivyo. Wanamuziki wa south africa ni mfano wa kuigwa kwa kujikubali na kutokubali kutumia western styles kumsifu Mungu . Mapambio yao ni ya ladha za utamaduni. kucheza kwao hakuna hata chembe ya umagharibi. kuvaa kwao pia katika nyimbo nyingi huvaa kiutamaduni. Solly ambaye mara ya kwanza aliibuka na Obrigado ambayo ni lugha ya hapo jirani Msumbiji alipokelewa vizuri sana. ndani ya hiyo album ya Obrigado ameimba pambio la kiswahili  linaloitwa ebaba pokea sifa. huwezi amini imebidi watu washangae jinsi alivyolipanga pambio hili na kuonekana kama wimbo mpya kabisa masikioni. Ubunifu wake wa hali yajuu sana ndiyo nguzo katika maonesho yake yakuvutia sana kwenye majukwaa. hufurahisha na huchangamsha sana akiwapo jukwaani.akiwashirikisha watazamaji wote. album iliyo fuata ameimba mwamba mwamba ambayo ni kiswahili. na kuna nyimbo nyingi kama wahamba nathi siyabonga na nyinginezo nyingi. Solly amestahili kabisa tuzo hii.

Keep it up baba Solly usilale wakilisha popote pale na karibu Tanzania...........

ANGALIA BAADHI YA TRACK ZA SOLLY HAPA CHINI


 STAGE YA SAMA SO MCHEZO


 OBRIGADO ALBUM YAKE SOLLY MAHLANGU


WAHAMBA NATHI YAKE SOLLY


JESO KONYAMA


SOLLY ft keke and zanele



Angalia hizi

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...