matukio burudani injili uimbaji maisha sanaa muziki maigizo habari maajabu vichekesho maendeleo mafanikio uchumi lugha maono mahubiri nyimbo biblia siasa

Apr 8, 2012

TAMASHA LA PASAKA 08/04/2012 NI LA KIHISTORIA-ANGALIA HAPA MATUKIO

 Kwanza mambo yalianza kwa kutengeneza stage ambayo iliwekwa katikati ya uwanja. Plan ni watu wote waweze kuona kwa urahisi.
JUU: REBECCA MALOPE AKIWA UWANJANI WAKATI WATU WAKIWA TAYARI WAMEKWISHA INGIA UWANJANI. ALIVAA KOFIA NA HAIKUWA RAHISI KUMTAMBUA                                    

 JUU PICHANI NI UMATI WA WATANZANIA KATIKA UWANJA WA KIMATAIFA WAKISUBIRI TAMASHA LA PASAKA KUANZA

JUU; CHRISTINA SHUSHO, UPENDO NKONE NA UPENDO KILAHIRO WAKIWASILI UWANJANI HUKU WAMESHIKILIA WATOTO WAO MIKONONI


 MWANAMAMA ROSE MUHANDO MUIMBAJI MKONGWE HAPA TANZANIA AKIINGIA UWANJANI HUKU AKIPUNGA MIKONO BAADA YA WATU KUMSHANGILIA SANA. ILIKUWA RAHA TUPU..........
                                           
 WANAMUZIKI WAWILI KUTOKA KENYA PEMBENI YA ROSE MUHANDO WA TANZANIA WAKIELEKEA KWENYE MAHEMA KATIKATI YA UWANJA TAYARI KWA SHUGHULI YA TAMASHA...............

 WATOTO WANAINGIA UWANJANI KUNOGESHA SIKUKUU YA PASAKA NDANI YA TAMASHA LA PASAKA







                                     









JUU; GLORIOUS CELEBRATION KAZINI WAKIIMBA WOZA WOZA NIGUSE PAMOJA NA UNAWEZA YESU..................ILIKUWA NZUUUUURI SANA

JUU : UPENDO KILAHIRO AKIIMBA ZINDONGA ZE ZIWELALE STAGINI

 

 JUU; JOHN LISU AKIIMBA JEHOVA YU HAI


                                      

JUU: ANASTAZIA MUKABWA NA KUNDI LAKE KUTOKA NCHINI KENYA WAKIMSIKILIZA MMOJA WA WAIMBAJI WAKATI WAO WAKIJIANDAA KUIMBA...............SHUGHULI INAENDELEA HAPA,,,,,,,//////////CHINI: MUKABWA NA ROSE WAKIIMBA VUA KIATU KWA PAMOJA.


                                      
 JUU: NI MKENYA AKIIMBA NYIMBO YA KIASILI KUTOKA KENYA

JUU PICHANI.NI REBECCA SASA AKIFANYA VITU VYA UKWELI. ALIWEZA KUIMBA NYIMBO ZAIDI YA SITA  NA KUFANYA SHOW ZA SARAKASI NA VIJANA WAKE HUKU AKIVALIA KIVAZI CHA KIASILI CHA AFRICA YA KUSINI. REBECCA HAKUPANDA KABISA JUKWAANI KWANI ALIONA JINSI AMBAVYO UMATI WA WATU UMEJAA ASINGEWEZA KUMPENDEZA KILA MMOJA HIVYO ALIISHIA KUIMBA UWANJANI AKIZUNGUKA HUKU NA HUKO ILI TU KUTAWALA JUKWAA VYEMA. MWISHONI AKASEMA MWAKA UJAO ATAKUJA TENA AKIPEWA MWALIKO, NA WAAFRICA NI WAMOJA NA KAMA IKIWEZEKANA ATANUNUA NYUMBA TANZANIA.
 JUU:

 CHINI; ROSE MUHANDO AKIIMBA UTAMU WA YESU AMBAO ULISIMAMISHA WATU WOTE UWANJANI. ROSE ANAPENDWA NA WATU WENGI MNO NDO MAANA WATU WENGI WALIPOMUONA WALIINUKWA KWA SHANGWE KUBWA. BIG UP ROSE.............


                                      
 CHINI PICHANI; EPHRAIM SEKELETI KUTOKA ZAMBIA LEO ALIIMBA LIVE NYIMBO MBILI IKIWA NI BARAKA ZAKO ZIWE NA MIMI NA NYINGINE MPYA KABISA AMBAYO IMEPOKELEWA VYEMA KABISA. SEKELETI KAONYESHA UKOMAVU MKUBWA SANA KWA UIMBAJI WAKE USIOKUWA NA CHENGA. SAUTI YAKE IMENYOOKA HAINA MAWIMBI
 CHINI NI UPENDO KILAHIRO NA DADA CHRISTINA SHUSHO AMBAO PIA WALIIMBA KWENYE TAMASHA .  WAMEONYESHA UKOMAVU MKUBWA SANA KATIKA FANI
chini; Alex Msama ambaye ndiye muandaaji wa shughuli nzima ya tamasha hili la pasaka 2012
Mambo mbalimbali yaliainishwa siku za usoni na Mratibu wa Matamasha wa Basata, Bashir Mashiri 'Ngosha', wakati Msama Promotions ikiwasilisha maombi ya kibali cha tamasha la Pasaka la mwaka huu.
Ni lile Tamasha la Muziki wa Injili ambalo huwika kila mwaka kipindi cha Pasaka, chini ya Uratibu wa Kampuni ya Msama Promotions na linatarajiwa kuingizwa kwenye Orodha ya matukio rasmi ya kitaifa chini ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).
Kampuni hiyo ambayo imekuwa ikiandaa tamasha hilo tangu mwaka 2000, kwa sasa inasubiri majibu ya tamasha la mwaka huu litakalofanyika Aprili 8 na 9.
Alisema uwezekano tamasha hilo likaingizwa kwenye orodha ya matamasha makubwa ya kitaifa, kutokana na maudhui na kukubalika kwake.
Na baada ya kuona tamasha hilo likipokelewa vizuri kila linapofanyika, baraza limeona ni bora likatambulika rasmi kitaifa.
Alisema mbali ya kukubalika kwa matamasha hayo, pia kitendo cha kutumia sehemu ya fedha kusaidia makundi maalumu kwenye jamii, ni jambo zuri la kuungwa mkono.
Naye mwenyekiti wa tamasha hilo, Alex Msama, alisema idadi ya watakaopewa msaada imeongezeka, kutoka wajane 50 hadi 100 mwaka huu.
Alisema wajane hao watapatiwa mitaji, wakati walemavu 150 watapata baiskeli huku idadi ya kusomesha watoto yatima kupitia tamasha hilo, pia ikiongezeka.
Kutokana na maandalizi ya tamasha hilo kuanza mapema, linatarajiwa kuwa tofauti na yaliyowahi kufanyika.

Angalia hizi

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...