matukio burudani injili uimbaji maisha sanaa muziki maigizo habari maajabu vichekesho maendeleo mafanikio uchumi lugha maono mahubiri nyimbo biblia siasa

May 21, 2012

Ripoti: wachawi wanaswa huko mwanza

 
Watu wawili waliofahamika kwa majina ya Masaganya Kalimanzila mwenye umri wa miaka 30 (mwanamke) na Chiza Juma (mwanaume),ambao wanajihusisha na shughuli za kishirikina (uchawi) wakazi wa wilayani Kasulu mkoani Kigoma, wamekamatwa majira ya saa 12 za alfajiri hapo jana katika kanisa la Ufunuo lililopo maeneo ya Butimba jijini Mwanza ambako walienda kwa ajili ya kuwachukua watu watatu waliotumwa na wakubwa zao mkoani Kigoma kwa ajili ya kwenda kuwatoa sadaka(kuwaua kwa njia ya uchawi).

Watu hao ambao wamesema wamesafiri kwa njia ya ungo toka kijiji cha Kaziramkunda wilayani Kasulu mkoani Kigoma hadi jijini Mwanza, wamesema walipewa amri na wakubwa wao wanaoishi chini ya maji ili kufika kanisani kuwachukua watu hao ambao hata hivyo hawakuwataja ili wakauliwe kwa njia ya kichawi na kufanywa kafara na mazindiko katika shughuli zao.Wakiwa kanisani hapo walikamatwa na wachungaji wa kanisa hilo ambao walifika asubuhi kama ilivyoada yao kwa ajili ya kufanya maombi na kujitakasa kwa ajili ya ibada.


Ingawa jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo,kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hakuna kipengele kinachotambua uchawi,hivyo hakuna kesi inayowakabili.dawa ni kuendelea kupiga maombi zaidi ili Mungu aendelee kuwafichua na kuwaponya ili waache tabia ambazo zimekuwa zikinyanyasa na kudidimiza hali za watanzania ambao hawajasimama katika neno.


 juu:Mchungaji wa kanisa la Ufunua Diana Bandele (kushoto) na Abigaili Zumaridi ambaye ni nabii wa kanisa hilo ambao waliwakuta wachawi hao kanisani mwao majira ya saa 12 kwani muda huo ni ada kwa wao kujitakasa kwaajili ya kuianza siku ya ibada.



juu ;  Wananchi na baadhi ya maafisa wa jeshi la polisi Mwanza wakiwa wamewazingira wachawi hao katika viwanja vya polisi Mwanza leo asubuhi katika kuchukuwa maelezo.


  juu: Pembejeo za kichawi mwanamke alisafiri kwa kutumia ungo na mwanaume akatumia mkuki na pembe.


 
juu ; Wakifanyiwa mahojiano,huku wakitazamwa na watu mbalimbali waliokusanyika hiyo jana alfajiri.

 SOURCES:  http://unclejimmytemu.blogspot.com/ AND http://www.gospelkitaa.blogspot.com/

Angalia hizi

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...