matukio burudani injili uimbaji maisha sanaa muziki maigizo habari maajabu vichekesho maendeleo mafanikio uchumi lugha maono mahubiri nyimbo biblia siasa

May 18, 2012

TANGAZO LA MKUTANO 13/6/2012-17/06/2012 SAA TISA ALASIRI

 
SOS Mission walikuwepo mwaka jana kwenye tamasha kubwa la aina ya la Campas Night lililokuwa na timu kubwa, wakiongozwa na kiongozi wao Past Johnnes mwaka huu wanakuja na mkutano mkubwa wa injili utakao fanyika hapa Dar kuanzia Tar 13-17 Jun mkutano huo umepewa jina la sherehe za ishara na miujiza. maanadalizi ya mkutano huo yanaendelea kwa kasi kwa kuandaa watenda kazi wengi. Timu ya maombi teyali wanaendelea na maombi katika kanisa la mito ya baraka pale Jangwani kila wiki, wachungaji na wahudumu wengine nao wanaendelea kuandaliwa ili kuhakikisha kuwa kila idara ina kaa vizuri.

 SOS watakaokuja Dar wanakadiliwa kuwa 200 hivi na watafanya uinjilisti mitaani kwa kutumia magari na helkopta kwa kutua kwenye openi na kuweza kufanya ushuhudiaji hivyo wanaobwa vijana waliookoka wanaoweza kutafsili kingeleza kuja kiswahili kujitokeza ili kuzunguka na timu hiyo na wengine watakuwa kwenye helkopta(haya ambao hamjawahi kupanda helkopta changamkia tenda) zaidi ya hapo wakati wa mkutano mtu atakyeleta watu 20 atapewa zawadi na watu hao watalipiwa nauli na mchungaji atakayelea watu 20 yeye atapewa zawadi ya vyombo vya mziki kwaajili ya huduma. hivyo jiandae kuleta watu uwezavyo ili ujinyakulie zawadi. na si hivyo tu wachungaji watapata kusaidiwa kielimu pia. ikiachilia uinjilisti utakao fanywa SOS band watakuwepo kutumbuiza siku zote za mkutano na waimbaji wengine wa hapa kwetu Tanzania watakuwepo kama Kinondoni Revival, Temeke Revival, the Repers ,Upendo Nkone, Christina Shusho, Bony Mwaitege, John Shabani na wengineo. wapendwa tunaobwa kuja na watu wasiookoka, wagonjwa na wenye matatizo mbalimbali ili wakutane na Mungu wao na kupokea miujiza yao na kama unataka kuwa mhudumu utawasiliana na no hapo chini.

SOURCE;http://johnshabani.blogspot.com/

Angalia hizi

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...