matukio burudani injili uimbaji maisha sanaa muziki maigizo habari maajabu vichekesho maendeleo mafanikio uchumi lugha maono mahubiri nyimbo biblia siasa

Nov 22, 2014

GEORGE NJABILI BONGE, MWIMBAJI WA GOSPEL AFARIKI DUNIA TAR 21 NOVEMBER 2014. NURU IKUTANGULIE MBELE YAKO GEORGE! TULIKUPENDA

MSIBA
Ilikuwa tarehe 21 november 2014 Majira ya asubuhi Mtumishi alipokuwa akijiandaa kwenda job ghafla alianguka na walipokuwa wakijaribu kuwahi hospital kwa ajili ya matibabu ndipo alipoiaga dunia njiani kuelekea hospitali. ni hisia kubwa kwa wale wote wapendao gospel songs kuondokewa na Nguli mahiri wa utungaji na uimbaji hapa nchini. Mr George Njabili Bonge alikuwa anaimba kwaya ya Lulu Mtoni evangelical ambapo alivuma sana kwa kuimbisha wimbo wa Around the corner Jesus is coming. Ujumbe huu ametuachia kwa kweli tutamkumbuka daima.
 
 Marehemu George Njabili na Mke wake wakati wa uhai wake akimuimbia Mungu nyimbo

Marehemu George akiwa katika moja ya matamasha ya uimbaji na kwaya yake. 

Akihudumu stejini kama ambavyo ilipasa mtumishi wa Mungu kufanya. hakika watu walibarikiwa na huduma yake. Mshumaa umefifia sasa. Mungu uhimidiwe kwa ajili ya George bONGE Njabili.

Sio muda mrefu tu uliopita George Njabili alikuwa amefungua bendi ambayo ilisha kuwa inashika kasi katika kufanya uinjilishaji. Mshumaa Umefifia sasa. Maono hayo alikuwa nayo siku ya tamasha la Rose Mhando pale Diamond jubilee kwenye album ya Pindo la Yesu Mr George Njabili aliimba live kabisa bila kutumia CD na bendi yake mpya na Mungu aliinuliwa. hakika George amefanya utumishi kati kati yetu.

Msiba huu umewagusa wengi sana. kwa Mujibu wa taarifa kutoka kwenye familia Mwili wa marehemu unapelekwa Tukuyu Mbeya kwa ajili ya kufanya taratibu ya masishi.

ANGALIA VIDEO HIYO HAPO CHINI UONE NYIMBO ALIYOIMBA AKIWA LULU MTONI EVANGELICAL CHOIR. AROUND THE CORNER JESUS IS COMING. 


Ilikuwa ni nyimbo ya muda mrefu ila aliimba kwa umahiri mkubwa sana. Mungu iweke na ipe nafasi roho yake katka ufalme wako. Amen

Angalia hizi

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...