matukio burudani injili uimbaji maisha sanaa muziki maigizo habari maajabu vichekesho maendeleo mafanikio uchumi lugha maono mahubiri nyimbo biblia siasa

Jun 30, 2015

FLORA MBASHA AONYESHA UKOMAVU SANA KATIKA LIVE MUSIC YA INJILI.

KATIKA UZINDUZI AMBAO AMEUFANYA FLORA MBASHA UBUNGO PLAZA TAREHE  14/06/2015

CHEKI HII VIDEO 

 

Kwanza iyelele team inampongeza huyu mwanamama kwa jinsi alivyofanya siku hiyo uzinduzi wa DVD yake pamoja na band yake mpya kabisa ambayo anaingia nayo kazini sasa aliimba kwa hisia kubwa akiomba Mungu ampe nguvu zaidi ya kuifanya kazi yake. Kiukweli alidhihirisha kuwa yeye ni mwanamuziki mzoefu na ambaye habahatishi katika kazi yake. Huyu ndiye Flora mpya kabisa alliyejaa upako kiukweli. Dvd ilienda kwa jina la Nipe nguvu ya kushinda.....

Picha na matukio haya yafuatayo yakionyesha ni jinsi gani tukio lenyewe lilivyofana. Angalia

 Flora Mbasha

 Makirikiri wakimsupport dada flora kwa kucheza katika onesho hilo. hawa nao kiboko!

 mgeni rasmi katika uzinduzi huu alikuwa ni mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo mheshimiwa Freeman Mbowe. hapa akiwa anasoma nyimbo zilizopo kwenye ile dvd ya flora



 Flora Mbasha


 hisia na machozi yaliyobubujikwa jukwaani hakika yalikuwa ni dalili ya upako aliokuwa nao siku hiyo dada flora
watu wakifuatilia kwa makini tukio zima la uzinduzi katika ukumbi wa ubungo plaza

Angalia hizi

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...